Home Azam FC AZAM FC YAMTABULISHA JONAS TIBOROHA

AZAM FC YAMTABULISHA JONAS TIBOROHA

 

UONGOZI wa  Azam FC, leo Agosti 16 umemtambulisha Mkurugenzi wa Masuala ya Mpira, Jonas Tiboroha ambaye atafanya kazi ndani ya timu hiyo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, katika ukumbi wa mikutano ulipo Mzizima, Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdukarim Amin amesema kuwa malengo makubwa ya timu hiyo ni kuzidi kujiimarisha katika kila sekta ili kuwa imara zaidi.

Amin amesema:-“Kwa muda mrefu wengi wamekuwa wakimtambua CEO peke yake pamoja na watendaji wengine lakini leo tunamtambulisha kwenu Mkurugenzi wa Masuala ya Mpira.

“Kazi kubwa ni kuona namna gani tunaweza kuwa imara na kuzidi kuboresha timu yetu kwa sababu anakuja kufanya kazi katika kuyafikia malengo ambayo tumeweka,” amesema.

Tiboroha ambaye amepewa dili la mwaka mmoja amesema kuwa amekubali kufanya kazi hapo kwa kuwa ni moja ya timu bora na yenye mipango makini.

“Nimekubali kuja kufanya kazi hapa kwa kuwa ni moja ya timu bora, kazi ambayo nakuja kuifanya  ipo kwenye mpango kazi,” .


SOMA NA HII  KUMEKUCHA FEI TOTO ATAKA KULIANZISHA TENA AZAM, ADAI HANA FURAHA