Home Yanga SC STRAIKA MPYA YANGA ASHTUA..FAMILIA YAKE WAFUNGUKA HAYA KUMUHUSU..

STRAIKA MPYA YANGA ASHTUA..FAMILIA YAKE WAFUNGUKA HAYA KUMUHUSU..


KLABU ya Yanga imesajili nyota wapya 11 wakiwamo mapro wa kigeni saba, lakini kuna straika mpya mzawa Athuman Yusuf aliyenaswa kutoka Biashara United, amemshtua kipa wa timu iliyoshuka daraja ya Gwambina, Ibrahim Isihaka, akisema kama jamaa atatuliza akili na kupambana, atatoboa Jangwani.

Yusuf ni kati ya wachezaji wazawa wanne walioongezwa Yanga cha msimu ujao wa Ligi Kuu Bara, akiwamo winga Dickson Ambundo, beki David Brayson na kipa aliyekuwa akicheza Burundi, Erick Johora akiwa mmoja ya wachezaji aliyeisaidia Biashara kumaliza nafasi ya nne ya Ligi Kuu na kukata tiketi ya michuano ya kimataifa, msimu huu ikishiriki Kombe la Shirikisho Afrika.

Straika huyo aliye kwenye orodha ya wachezaji 28 wanaoondoka leo kwenda Morocco kuweka kambi, aliwahi kuwika Mbao FC na Singida United kabla ya kunaswa na Biashara na msimu huu Yanga kumdaka na jambo hilo limemshtua kipa huyo wa Gwambina, aliyemuonya mapema ili atoboe Yanga.

Isihaka ambaye ni mdogo wa Yusuf, alisema amejisikia furaha kuona ndugu yake amesajiliwa Yanga kwani ni timu kubwa na kila mchezaji anatamani kuichezea.

‘‘Kwetu kama familia tumefurahi sana kuona ndugu yetu amesajili Yanga, kujiunga kwake kwa klabu kubwa inashtua kwa kuamini atakabiliwa na changamoto kubwa, lakini kwa kipaji kikubwa cha soka alichonacho akikomaa ni rahisi kutoboa, kwani unaonekana zaidi kuliko ukiwa kwingine, ndio maana kila mchezaji huwa anatamani kuichezea Yanga na hata Simba au Azam, hii kwetu ni heshima kubwa,” alisema Isihaka.

Kipa huyo alisema kwa sasa kaka yake anatakiwa kupambana ili kuweza kupata namba ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza.

‘‘Yanga ni kubwa, anatakiwa kujua hilo kwani pale kuna wachezaji wakubwa wenye viwango bora sana hivyo kwake anatakiwa kujituma sana kuanzia mazoezini na kwenye mechi, bahati nzuri nimezungumza naye na kila mara namsisitiza apambane ili kumridhisha kocha aweze kumpa nafasi ya kucheza. anapenda kujituma. Sina shaka naye.”

SOMA NA HII  JULIO : WAAMUZI BONGO 'WANAIKOSTI' YANGA KIMATAIFA...VIONGOZI WAO WAACHE UJANJA UJANJA...