Home Uncategorized BEKI WA ZAHERA YANGA MGUU NJE MGUU NDANI

BEKI WA ZAHERA YANGA MGUU NJE MGUU NDANI

BEKI wa Yanga, Paul Godfery ‘Boxer’ kipenzi cha Mwinyi Zahera kwa sasa haelewi chochote kinachoendelea juu yake msimu ujao kutokana na kutopewa taarifa zozote ndani ya klabu hiyo.

Boxer msimu uliopita alionyesha uwezo mkubwa kwenye mechi zake alizocheza ambapo alikuwa mhimili kwa upande wa mabeki wa Yanga licha ya kupandishwa kutoka timu ya vijana.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Boxer alisema kuwa kwa sasa hajui hatma yake ndani ya Yanga na nini kinachoendelea juu yake.

“Ndugu yangu nashukuru Mungu nipo salama ila kwa upande wa mkataba wangu ndani ya Yanga sijui chochote kwa kweli, niponipo tu kwa sasa,” alisema Boxer.

SOMA NA HII  BABA SAMATTA AIBUKA NA UJUMBE MWINGINE KWA MWANAYE