Home news PAMOJA NA KUICHAPA ASEC JUZI…PABLO ASHINDWA KUJIZUIA KUHUSU KAGERE…ZIMBWE JR NA NYONI...

PAMOJA NA KUICHAPA ASEC JUZI…PABLO ASHINDWA KUJIZUIA KUHUSU KAGERE…ZIMBWE JR NA NYONI WATIA NENO…


JUZI kwenye Uwanja wa Mkapa, Simba ilianza vizuri mechi ya Kombe la Shrikisho Afrika kwa kuifumua bao 3-1 Asec Mimomas ya Ivory Coast na kushika nafasi ya pili kundi D lenye timu nne.

Mechi nyingine ya kundi hilo ilikuwa kati ya Rs Berkane ya Morocco na US Gendarmerie ya Niger iliyomalizika kwa Berkane kupata ushindi wa bao 5-3 nyumbani.

Kocha mkuu wa Simba, Pablo Franco aliweka wazi kuwa; “Ilikuwa ni mechi ngumu kutokana na ubora wa wapinzani wetu kila eneo lakini tulihitaji ushindi huu wa nyumbani ili kuanza vizuri hatua hii.”

“Tulitengeneza nafasi nyingi hususani kipindi cha kwanza zikiwemo zile za Banda na Meddie Kagere walizokosa lakini tulipata bao moja tu na hivyo ndivyo mpira ulivyo. Tulivyoenda kwenye vyumba vya kubadilishia nguo niliwasihi wachezaji kuongeza umakini kwenye kujilinda na kutumia nafasi vyema za kufunga maana kwenye michuano kama hii unahitaji kuwa makini zaidi, tulifanya makosa kidogo wakasawazisha tukaanza kuwashambulia tena tukapata Penalti na bao la tatu.” alisema Pablo

Kocha huyo alisema ushindi huo umewapa mwanga bora kuelekea michezo miwili ijayo ambayo Simba itakuwa ugenini Niger Jumapili Februari 20, dhidi ya US Gendarmarie kabla ya kwenda Morocco kuivaa Berkane Februari 27. “Siku kadhaa zilizopita tulipita katika kipindi kigumu, lakini leo (juzi), wachezaji wameonesha viwango bora nadhani hii itatusaidia kuelekea mechi zijazo ambazo zitakuwa ngumu pia,” alisema Pablo.

TSHABLALA, NYONI

Katika hatua nyingine Nahodha msaidizi wa Simba, Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ na kiraka Erasto Nyoni wamewatoa wasiwasi mashabiki juu ya ubora wa timu yao katika michuano yote inayoshiriki.

“Mchezo ulikuwa mgumu, Asec sio timu mbaya, tulijianda vizuri na tumepata alama tatu. Tumejipanga kufanya vizuri kotekote na nawaomba mashabiki wetu waendelee kutusapoti mambo mazuri yanakuja,” alisema Nyoni ambaye ni kiraka aliyedumu kwenye fomu kwa miaka mingi pengine kuliko wachezaji wote waliopo kwenye kikosi cha Simba kwa sasa na Taifa Stars.

Naye Tshabalala alisema kuwa; “Kila mtu alihitaji alama tatu kwenye mchezo huo, hakuna anayependa kupoteza mchezo, tunapambana kwaajili ya timu na tunaamini tutaendelea kupata matokeo kikubwa mashabiki waendelee kutusapoti,” alisema Tshabalala.

SOMA NA HII  BAADA YA KUISAIDIA YANGA KUWA MABINGWA...DICKSON JOB AIBUKA NA HILI JIPYA TENA...ASISITIZA NI LAZIMA IWE HIVYO...

Simba imesisitiza kwamba inakwenda kucheza mechi mbili za ugenini kwa umakini mkubwa wakizingatia ugumu wa soka la Morocco na Niger na jinsi klabu hizo zilivyojipanga msimu huu haswa nyumbani.