Home Uncategorized YANGA YASHUSHA PRESHA KISA SIMBA, SASA KAZI ITAKUWA NAMNA HII

YANGA YASHUSHA PRESHA KISA SIMBA, SASA KAZI ITAKUWA NAMNA HII

KOCHA Mkuu wa Yanga, Luc Eymael amesema kuwa siku zilizobaki zinatosha kukiandaa kikosi chake kwa ajili ya mchezo wa Machi 8 dhidi ya Simba utakaochezwa Uwanja wa Taifa.

Hii itakuwa ni dabi ya kwanza kwake tangu alipotua Dar akichukua mikoba ya Mwinyi Zahera.

Eymael amesema:” Mchezo wetu dhidi ya Simba sio mwepesi lakini tutapambana kwa siku ambazo zimebaki ili kupata matokeo mazuri hilo linawezekana na wachezaji wangu nimewaambia kwamba wanapaswa washushe presha kila kitu kinawezekana,”.

Zimbekaki tatu kwa watani hawa wa jadi kukutana Uwanja wa Taifa mchezo wa pili wa Ligi Kuu Bara, ule wa kwanza uliochezwa Januari 4, ngoma ilikuwa 2-2.

Mchezo wao wa mwisho kabla ya kuivaa Simba ilishinda mabao 2-0 mbele ya Mbao FC huku wafungaji wakiwa ni David Molinga na Patrick Sibomana huku Simba nao wakishinda mchezo wao wa mwisho mbele ya Azam FC mabao 3-2.

SOMA NA HII  JUVENTUS KUMNYAKUA DE GEA