Home Habari za michezo BAADA YA KUONA HAKUNA WA KUZUIA…YANGA WALIFUATA KOMBE LAO LA UBINGWA MBEYA...

BAADA YA KUONA HAKUNA WA KUZUIA…YANGA WALIFUATA KOMBE LAO LA UBINGWA MBEYA KWA MIKOGO KAMA YOTE….


Kikosi cha Timu ya Wananchi Yanga kimetua salama Jijini Mbeya kwa ajili ya kukamilisha michezo ya ugenini kwenye mbilinge mbilinge za Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara msimu huu ambapo awamu hii watamaliza na Mbeya City mtanange utakaopigwa dimba la Kumbukumbu ya Sokoine.

Mchezo huo utachezwa Juni 25, siku ya Jumamosi ambapo kwenye mechi hiyo Yanga itakabidhiwa taji la Ligi Kuu kwa mara ya kwanza tangia msimu wa 2017 kwani kipindi chote ubingwa ulikuwa unaenda kwa Simba SC.

Wanakabidhiwa ubingwa kabla Ligi haijaisha baada ya kuvuna alama ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote si Simba nafasi ya pili, Geita Gold au Azam FC.

Bahati iliyoje kwa Yanga, baada ya kukaa bila Kombe kwa takribani miaka minne sasa msimu huu pia Yanga watachukua ubingwa ambalo ni Kombe jipya kwao ambalo lilitambulishwa na Bodi ya Ligi Kuu nchini chini ya Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), Steven Mnguto na Katibu Almas Kasongo.

Baada ya mchezo huo, Yanga itakamilisha ratiba ya msimu huu jijini Dar es Salaam ambapo watacheza na Mtibwa Sugar uwanja wa Mkapa.

SOMA NA HII  KWISHA KAZI....VIGOGO WAZITO YANGA SC WAITIBULIA AZAM FC KWA FEI TOTO...