Home Habari za michezo BAADA YA KUONA WAARABU WENZAO WAMEPASUKA 4-0…AL AHLY KUIKABILI YANGA KININJA NINJA…

BAADA YA KUONA WAARABU WENZAO WAMEPASUKA 4-0…AL AHLY KUIKABILI YANGA KININJA NINJA…

Habari za Michezo leo

Kocha Mkuu wa Al Ahly, Marcel Koller amewataka wachezaji wa kikosi hicho kuongeza umakini zaidi wakati watakapopambana na Yanga katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika kuhitimisha makundi utakaopigwa leo kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Cairo.

Akizungumza kutoka Misri, Koller alisema, mchezo huo ni muhimu kwa timu zote katika harakati za kuwania kuongoza kundi ingawa kwa jinsi alivyoiona mechi ya Yanga na CR Belouizdad amegundua ana kazi kubwa ya kufanya kuizuia.

“Walicheza vizuri mechi yao ya mwisho hivyo ni lazima tucheze kwa tahadhari kubwa ili kupata matokeo chanya, sitaki kuzungumzia mchezaji mmoja mmoja kwa sababu nilichokiona wakishambulia wako pamoja sawa na kwenye kuzuia pia,” alisema.

Koller aliongeza, mchezo wao wa juzi wa Ligi walioibuka na ushindi wa mabao 5-1, dhidi ya Baladiyat El Mahalla umekuwa na tija kwao kwani baadhi ya wachezaji waliokuwa majeruhi wamepata nafasi ya kurejea katika hali zao za kawaida tofauti na mwanzo.

Mchezo huo ni wa kukamilisha ratiba tu kutokana na zote kufuzu hatua ya robo fainali ingawa vita kubwa iliyopo ni timu ipi itamaliza kinara wa kundi ‘D’ kwa sababu Al Ahly inaongoza ikiwa na pointi tisa huku kwa upande wa Yanga ina nane.

Mechi ya kwanza iliyochezwa jijini Dar es Salaam, timu hizo zilifungana bao 1-1, Desemba 2, mwaka jana.

SOMA NA HII  KOCHA MPYA SIMBA HUYU HAPA...KASHINDA LIGI YA MABINGWA NA TP MAZEMBE..KOCHA WA BILION 1.17 APIGWA CHINI