Home Habari za michezo IHEFU, MBEYA KWANZA NA SINGIDA FG KUBADILISHWA MAJINA…MCHONGO WOTE UKO HIVI…

IHEFU, MBEYA KWANZA NA SINGIDA FG KUBADILISHWA MAJINA…MCHONGO WOTE UKO HIVI…

Habari za Michezo

Kwa mujibu wa ripoti mbalimbali zinasema kuwa klabu ya Ihefu yenye maskani yake mkoani Singinda inampango wa kubadilisha jina na kuwa Singida Leopards FC kuanzia msimu ujao.

Ihefu kwa sasa inatumia uwanja wa CCM Liti na wataanza kuutumia kwenye mchezo wao wa Ligi dhidi ya Mashujaa ya mkoani kigoma.

Hata hivyo ripoti zinaeleza klabu ya Mbeya kwanza ipo mbioni kununuliwa na kubadilishwa jina kuwa Ihefu na watautumia uwanja wa Ubaruku uliopo Mbarali Jijini Mbeya.

Wakati huo huo Singida Fountain Gate itabadili jina pia na kuwa Fountain Gate Academy na maskani yake yatakuwa mwanza kwenye uwanja wa Fountain Gate uliopo Gwambina mara baada ya uwanja huo kufanyiwa marekebisho.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI