Home Habari za michezo SIMBA WANAPASWA KUJUA UKWELI HUU KABLA YA MECHI YA KESHO…WAKIZUBAA IMEKULA KWAO..

SIMBA WANAPASWA KUJUA UKWELI HUU KABLA YA MECHI YA KESHO…WAKIZUBAA IMEKULA KWAO..

FT:- SIMBA 6-0 TRA

Nchi ina furaha kwa sasa baada ya timu moja ambayo ni Yanga kuingia hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Furaha hiyo inaweza kuongezeka zaidi kesho ikiwa Simba itaibuka na ushindi dhidi ya Jwaneng Galaxy ya Botswana kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa kuanzia saa 1:00 usiku.

Historia inaonyesha Simba imekuwa na historia nzuri ya kupata ushindi katika mechi kama hizo ambazo huwa inatakiwa ipate ushindi iweze kutinga hatua ya robo fainali iwe ya Ligi ya Mabingwa Afrika au Kombe la Shirikisho Afrika.

Msimu wa 2018/2019, Simba ilikutana na hitaji kama hilo katika mechi ya mwisho ya makundi dhidi ya AS Vita na ikapata ushindi wa mabao 2-1 na msimu wa 2020/2021 ikaichapa tena AS Vita kwa kichapo cha mabao 4-1 katika mechi ambayo ilikuwa na hitaji kama la kesho.

Msimu uliofuata, Simba ikakutana tena na mazingira kama hayo kwenye Kombe la Shirikisho Afrika ikapata ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Gendarmerie ya Niger na msimu uliopita ikatoa kichapo kizito cha mabao 7-0 kwa Horoya katika mechi ya mwisho na kutinga robo fainali.

Ushindi huo wa Simba mara zote hizo haukutokea kwa bahati mbaya bali ilifanya maandalizi ya kina ya kimbinu, kiufundi na kiutawala yaliyochagizwa na sapoti kubwa ya mashabiki ambayo yaliifanya itimize kile ambacho kilitarajiwa na wengi.

Hili ndilo jambo pekee ambalo linapaswa kufanywa kwa ajili ya mechi dhidi ya Jwaneng Galaxy hapo kesho ili Simba iweze kusonga mbele badala ya kuamini itapata ushindi kirahisi kisa kuna historia ya kufanya vizuri nyuma ambayo wanayo.

Kimahesabu, Jwaneng Galaxy inaweza kuingia robo fainali kama itaifunga Simba na Wydad ikapoteza mbele ya Asec Mimosas hivyo hapana shaka itapambana vilivyo katika mechi hiyo badala ya kucheza kwa ajili ya kukamilisha ratiba tu.

Na Simba inatakiwa kukumbuka kwamba msimu wa 2021/2022 hao Jwaneng Galaxy walifanya isiingie makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuwafunga mabao 3-1 palepale Benjamin Mkapa.

SOMA NA HII  ILE ISHU YA MSUVA KUTAKIWA NA TP MAZEMBE KUMBE IKO HIVI AISEE...WENYEWE WAFUNGUKA KILA KITU...