Home Uncategorized WINGA AS VITA: NIMEFANYA MAZUNGUMZO NA YANGA

WINGA AS VITA: NIMEFANYA MAZUNGUMZO NA YANGA


TUISILA Kisinda winga anayekipiga ndani ya Klabu ya AS Vita ya Congo amesema kuwa amefanya mazungumzo na viongozi wa Yanga ambao wanahitaji kuipata saini yake.

Winga huyo anatajwa kuwa Kwenye mapendekezo ya Kocha Mkuu wa Yanga, Luc Eymael hivyo mambo yakiwa sawa anaweza kuibuka msimu ujao.

Tuisila amesema:- “Tayari nimefanya mazungumzo na Yanga kuhusu suala la wao kunisajili ili niitumikie timu yao msimu ujao.


 “Bado mazungumzo hayajakamilika kwa sasa na nina amini kwamba mambo yakiwa sawa nitajiunga nayo ili kuitumikia.”

Hersi Said Mkurugezi wa Uwekezaji wa GSM aliweka wazi mpango wa kampuni hiyo inayoidhamini Yanga kwenye masuala ya usajili kuwa muda wa usajili ukifika mambo yatakuwa wazi.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA GAZETI LA SPOTI XTRA KATIKA UKURASA WA MBELE LEO JUMAPILI