Home Uncategorized KISSU ATAFUTIWA MBADALA WAKE NDANI YA AZAM FC

KISSU ATAFUTIWA MBADALA WAKE NDANI YA AZAM FC


 DANIEL Mgore, kipa namba moja ndani ya Biashara United jina lake limeshikiliwa na Kaimu Kocha Mkuu wa Azam FC, Vivier Bahati raia wa Burundi ili aibuke ndani ya kikosi cha matajiri hao wa Dar kumpa changamoto, David Kissu.

Habari zinaeleza kuwa Mgore aliwekwa kwenye rada za Azam FC msimu uliopita kabla ya Aristica Cioaba ambaye alifutwa kazi Novemba 26 kupendekeza jina la Kissu hivyo kuondoka kwake kutafungua milango  kwa kipa huyo mzawa kuibuka ndani ya Azam FC.


Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa suala la usajili lipo ndani ya timu hiyo ila lipo mikononi mwa kocha ambaye yeye anajua anahitaji nini.


“Kuna uhitaji ndani ya timu na tutasajili lakini kwa kutegemea ripoti ya mwalimu, hivyo kwa kuwa amekaa na timu muda mrefu na anajua wapi kuna mapungufu basi atakuwa na jukumu la kupendekeza majina ambayo yatafanyiwa kazi,” amesema.


Kwa sasa Azam FC imeshampata kocha mpya ambaye ni George Lwandamina aliyetua Bongo usiku wa kuamkia leo akitokea nchini Zambia.


Timu hiyo kwa sasa ipo Mwanza ambapo imeweka kambi kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Gwambina FC utakaochezwa Desemba 7, Uwanja wa Gwambina Complex.


Habari zinaeleza kuwa makosa anayoyafanya Kissu ni sababu ya timu hiyo kuhitaji kipya mwingine ambaye atakuwa sambamba na Kissu katika kuweka lango salama.


Ikiwa imecheza mechi 13, zote langoni alianza Kissu na amefungwa jumla ya mabao saba.

SOMA NA HII  GAMONDI AFUNGUKA HALI WALIOPITIA KWA COASTAL UNION NI BALAA