Home Habari za michezo GAMONDI AFUNGUKA HALI WALIOPITIA KWA COASTAL UNION NI BALAA

GAMONDI AFUNGUKA HALI WALIOPITIA KWA COASTAL UNION NI BALAA

Habari za Yanga SC

KOCHA Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi  ameweka wazi kuwa mechi dhidi ya Coastal Union ilikuwa ngumu tofauti na alivyokuwa akifikiria, lakini amefurahi kwa ushindi huku akisema malengo yao msimu huu ni kuona wanatetea ubingwa.

Yanga ilikomba pointi sita katika michezo miwili  dhidi ya watani zao wa jadi Simba kwenye mchezo wa Kariakoo Dabi na Coastal Union.

Baada ya dakika 90 ubao ulisoma Simba 1-5 Yanga. Pointi tatu kibindoni na kutibua rekodi ya Simba kucheza mechi saba za msimu wa 2023/24 bila kufungwa kuendelea katika mchezo wa juzi dhidi ya Coastal Union kwa bao 1-0.

Kocha Gamondi  alisema wanatambua kwamba kazi kubwa kwenye mechi zao zote ni kusaka ushindi wakibadili mbinu kulingana na mchezo husika.

Alisema wamefanikiwa kupata pointi sita katika michezo miwili mfululizo, kila mchezo unakuja kulingana na aina ya wapinzani ambao anakutana nao.

“Tunatambua namna ushindani ulivyo hilo lipo wazi hivyo tunaingia uwanjani tukiwa na mpango kazi wa kusaka ushindi, kikubwa ni kuona kwamba tunacheza vizuri na kuwapa burudani mashabiki wetu  wanajitokeza uwanjani. Wazidi kuwa pamoja nasi kazi bado ipo na tunaamini tutafanya vizuri,” alisema Gamondi.

Akizungumzia mchezo huo alisema mechi ilikuwa ngumu niwapongeze wachezaji wachezaji wamecheza vizuri na mabeki wa Coastal Union walicheza vizuri kipindi cha keanza.

Alisema amefurahi kupata ushindi na walifanikiwa kutawala mchezo kipindi cha pili licha ya dakika 45 ya kwanza walipaswa kushinda .

“Niwapongeze vijana walipambana kwa sababu tulitoka kwenye mechi ngumu na kushinda bao 5-1 baada ya siku mbili tulikuwa na mechi na Coastal Union na kupata matokea mazuri,” alisema Gamondi.

Nahodha  wa Yanga, Bakari Mwamnyeto amefunguka kudai kubwa uchovu wa safari imekuwa sababu kubwa ya kuwa mchezo wao na Coastal Union kuwa mgumu.

Mwamnyeto alisema ilikuwa mechi ngumu lwa sababu wachezaji walikuwa na uchovu wa safari na kushindwa kuonyesha kiwango kizuri.

Alisema kikubwa wamefanikiwa kuvuna alama tatu ugenini ambazo ni muhimu kwao kuendelea kujiimarisha katika msimamo wa ligi hiyo.

“Kulikuwa na mabadiliko kidogo ndani ya kikosi. Mechi ilikuwa ngumu wachezaji tulikuwa na uchovu wa safari hali ambayo hatukuonyesha ubora wetu,” alisema Mwamnyeto.

Aliongeza kuwa anafurahi kupata alama tatu katika uwanja ambao umemtoa kisoka na nyumbani kwao kuhakikisha wanaendelea kupambana kwa kila mechi.

Naye Kocha wa Coastal Union, Fikiri Elias, alisema kilichowabeba Yanga ni ubora wa kikosi chao na kucheza kwa ushirikiano.

“Nawapongeza vijana wangu kwa kuweza kupambana kuhakikisha wanawazuia vizuri na kufanya kufungwa idadi chache ya mabao, wapinzani wetu wanakikosi kizuri na bora na hicho ndio walituzidi,” alisema.

Kocha huyo alisema wanaendelea kujifua kuhakikisha wanafanya mizuri katika michezo ijayo, anaamini anakikosi bora kitakachoweza kufanya vizuri katika ligi hiyo.

SOMA NA HII  GAMONDI AFUNGUKA KUHUSU MASTAA HAWA KUKOSA WAPINZANI KIKOSINI