Home Uncategorized MUUAJI WA SIMBA APANIA KUWAUMBUA TENA LEO UHURU

MUUAJI WA SIMBA APANIA KUWAUMBUA TENA LEO UHURU

MSHAMBULIAJI wa Mwadui FC, Gerald Mdamu amesema kuwa akipata nafasi leo ya kuanza dhidi ya Simba atapambana kuipa ushindi timu yake ili isonge hatua ya 16 kwenye hatua ya kuwania Kombe la Shirikisho utakaochezwa Uwanja wa Uhuru.
Mdamu aliifunga Simba walipokutana kwenye mechi ya Ligi Kuu Bara zilipokutana Uwanja wa Kambarage na leo watakutana na Simba Uwanja wa Uhuru kwenye mchezo wa hatua ya 32 bora.
Akizungumza na Saleh Jembe, Mdamu amesema kuwa wanatambua mchezo wao dhidi ya Simba utakuwa mgumu ila wamejipanga kupata ushindi ili kufikia malengo waliyojiwekea.
“Tumepangwa na Simba na tunatambua kwamba wana hasira kutokana na kwamba tuliwafunga kwenye mechi yao tulipokutana nao kwenye mchezo wa ligi, tutapambana kushinda mashabiki watupe sapoti,” amesema.
SOMA NA HII  KIKOSI CHA SIMBA DHIDI YA COASTAL UNION