Home Uncategorized RASMI, KOCHA YANGA KUIBUKA BONGO KESHO

RASMI, KOCHA YANGA KUIBUKA BONGO KESHO


KOCHA Mkuu wa Yanga, Luc Eymael anatarajiwa kutua kesho kwa ajili ya kuendelea kibarua chake majira ya saa 7:20 mchana.

Eymael aliibukia Ubelgiji baada ya Serikali kusimamisha masuala ya michezo kutokana na janga la Virusi vya Corona, Machi 17 alitarajiwa kurudi Juni 7 alikwama kutokana na kushindwa kukamilisha taratibu za usafiri.

“Nilipanga kurudi Juni 7 ila kuna mambo hayakukamilika kwa upande wa usafiri, kwa sasa ninatarajia kurejea rasmi Juni 10 kuendelea na majukumu yangu,” amesema.

Yanga ilianza mazoezi Mei 27 chini ya Kocha Msaidizi, Charles Mkwassa, itaendelea na mechi za ligi, Juni 13 ambapo itamenyana na Mwadui FC.

SOMA NA HII  KAZE ATANGAZA HALI YA HATARI YANGA