Home Uncategorized SIMBA YATAJA SABABU YA KUIFUNGA MWADUI FC LEO

SIMBA YATAJA SABABU YA KUIFUNGA MWADUI FC LEO


HAJI Manara Ofisa Habari wa Simba amesema kuwa sababu kubwa ya Simba kushinda mchezo huo ni kuongeza nguvu kwenye mradi wao wa kuingiza mashabiki wengi.

Uwanja wa Uhuru, majira ya saa 10:00 jioni, leo Simba itashuka kazini kumenyana na Mwadui FC ya Shinyanga kwenye mchezo wa hatua ya 32 bora na atakayechapwa anatolewa kwenye reli jumla.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram ametaja sababu hizi zitakazowafanya washinde mchezo wa leo:-“Leo tunacheza na Mwadui FC kwenye kombe la Shirikisho la Azam,tunawaheshimu na tunajua ugumu wao but (lakini) Simba kwa ukubwa wake haipaswi kuihofia timu yoyote Bongo.

“Na ktk hili niseme very clear (wazi) bila kupepesa macho,
Mradi wetu wa kuingiza Washabiki wetu ktk mfumo rasmi wa kuwatambua kwa kadi ili ufanikiwe ni lazma uendene na matokeo mazuri ya uwanjani.


“Kwa kifupi bila kushinda michezo kama hii ni ngumu sana kwa project (mradi) kama hii kutusua!!’


Wanasimba wanaujua uwezo wa wachezaji wetu na Insha’Allah tutashinda jioni pale Taifa,” amesema. 

SOMA NA HII  UWEZO WA PHIRI KUELEKEA DABI YA KARIAKOO