Home Habari za michezo PAMOJA NA ‘KUWAZAGAMUA’ WASUDAN JUZI…MASTAA YANGA WAPEWA ONYO KWA NAMUNGO…

PAMOJA NA ‘KUWAZAGAMUA’ WASUDAN JUZI…MASTAA YANGA WAPEWA ONYO KWA NAMUNGO…

Habari za Yanga

Baada ya kurejea nchini wakitokea Rwanda, Kocha Mkuu wa Young Africans, Miguel Angel Gamondi amewataka wachezaji wake kutobweteka na ushindi walioupata dhidi ya Al-Merrikh na badala yake waelekeze nguvu na akili zao kwenye mechi yao ya Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Namungo FC.

Young Africans itashuka katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi kesho Jumatano (Septemba 20) kuikaribisha Namungo FC katika mechi hiyo ya Ligi Kuu, ikitoka kuibanjua Al-Merrikh ugenini mabao 2-0 kwenye mechi ya raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika kuwania kufuzu hatua ya makundi.

Akizungumza baada ya timu hiyo kutua nchini ikitokea Rwanda ilipochezwa mechi yao dhidi ya Al-Merrikh ya Sudan, Gamondi amesema amewataka wachezaji wake kujiona ni bora kuliko timu nyingine baada ya kufanikiwa kupata ushindi dhidi ya Wasudan hao, lakini hawapaswi kujisahau kuelekea mechi yao ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Amesema katika mchezo huo walicheza vizuri na kutengeneza nafasi nyingi kwa kupata ushindi wa mabao 2-0 mbele ya timu nzuri na sasa wachezaji wanatakiwa kusahau matokeo hayo na kujipanga kwa mechi ijayo ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Tunafuraha kwa matokeo tuliyopata Rwanda, wachezaji walicheza vizuri tumepata nafasi nyingine, lakini sasa tunaangalia mechi iliyopo mbele yetu kuhakikisha tunaendelea pale tulipoishia kwa kutafuta ushindi wa idadi kubwa ya mabao.

“Nimeongea na wachezaji kuhakikisha wanasahau matokeo ya mechi zilizopita na kuingia uwanjani kucheza kwa tahadhari kubwa, kupata matokeo mazuri dhidi ya Namungo FC.” amesema kocha huyo.

SOMA NA HII  KIMEUMANA YANGA LEO HUKO UGENINI CAFCL