Home Habari za michezo KUNA NINI SINGIDA….?..KOCHA MPYA ADAIWA KUTIMKA….MASTAA HAWA WATAJWA…

KUNA NINI SINGIDA….?..KOCHA MPYA ADAIWA KUTIMKA….MASTAA HAWA WATAJWA…

Habari za Michezo

Kocha wa Singida Ernst Middendorp ameripotiwa kung’atuka klabuni hapo ikiwa ni chini ya mwezi tu tangu ashike hatamu ya kukinoa kikosi hicho huku aliyekuwa kocha msaidizi Mathias Luke akirejeshwa klabuni hapo kushika hatamu kama kocha wa muda.

Inaelezwa kocha huyo ametofautiana na bosi wa klabu hiyo aliyeripotiwa kuhoji kwanini kocha huyo hakuwapanga baadhi ya wachezaji kwenye mchezo dhidi ya Future FC ambao klabu hiyo ilishinda 1-0 na kuamua kutimka akidai hawezi kuingiliwa majukumu kwa kuwa anaamini anachokifanya.

Hata hivyo Afisa Habari wa Singida Big Stars, Hussein Masanza akijibu kuhusu kung’atuka kwa Mjerumani huko amesema “Kocha Ernst amepata dharura na ameondoka kwa dharura”

Masanza ametoa ufafanuzi huo leo akiwa katika dimba la Uhuru Dar es Salaam ambako kikosi cha Singida Fontaine Gate FC kinaendelea kujifua.

SOMA NA HII  MOHAMMED HUSSEIN "TSHABALALA"...NALIAMINIA JESHI LANGU...MECHI NA UGANDA TUTASHINDA