Home news WAKATI SIMBA WAKIENDELEA KUHANGAIKA NA SAKATA LA GSM..SENZO AIBUKA NA HILI YANGA…

WAKATI SIMBA WAKIENDELEA KUHANGAIKA NA SAKATA LA GSM..SENZO AIBUKA NA HILI YANGA…


SENZO Mbatha, Mtendaji Mkuu wa Yanga SC amebainisha kwamba hawana presha na watani zao wa jadi, Simba kuelekea kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuchezwa Desemba 11, mwaka huu.

Akizungumza na Gazeti la  Spoti Xtra, Mbatha alisema kuwa wanatambua kuhusu mchezo huo kwa kuwa upo kwenye ratiba, hivyo watafanya maandalizi mazuri ili kupata ushindi.

“Ipo wazi kwa muda mrefu kwamba lazima tutakutana na Simba kwenye mechi ya ligi, hivyo hakuna presha kuelekea mchezo huo, kila kitu kinakwenda sawa na maandalizi yake ni kama ilivyo kwenye michezo mingine.

“Mwendo ambao tunakwenda nao ninaamini kwamba mashabiki wanaona, hivyo hakuna haja ya kuwa na mashaka

juu ya uwezo wa wachezaji wetu ambao wapo kwani kila mmoja anafanya kazi kwa umakini katika kutimiza majukumu yake,” alisema Mbatha.

SOMA NA HII  ULE MPANGO WA AKPANA NA KAPAMA KUTEMWA SIMBA...KOCHA MAKI AKUBALI YAISHE..ATOA TAMKO HILI JIPYA...