Home Habari za michezo SIMBA WATAMBA , YEYOTE AJE HAKUNA MPINZANI TENA

SIMBA WATAMBA , YEYOTE AJE HAKUNA MPINZANI TENA

KIKOSI CHA SIMBA SAFARINI KUELEKEA MOROCCO...WATUMIA MBINU HII KUWACHANGANYA WAARABU

KIKOSI cha Simba kipo siku za mwisho mwisho za kambi ya maandalizi ya msimu mpya iliyopo Uturuki na Jumatatu ijayo inatarajiwa kurejea nchini, huku wachezaji, benchi la ufundi na hata viongozi wakitamba kwamba chama limeiva na wapinzani waletwe tu waonyeshwe.

Simba iliyosajili jumla ya wachezaji 29, wakiwemo 10 wapya na benchi la ufundi na baadhi ya viongozi wa juu wakiongozwa na Mwenyekiti wa klabu, Murtaza Mangungu na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Salim Abdallah ‘Try Again’ wanatarajia kuanza safari ya kurejea nchini mapema wiki ijayo ili kuwahi Tamasha la Simba Day litakalofanyika Agosti 6 kisha kugeukia mashindano.

Simba ikimalizana na tamasha hilo la msimu wa 15 tangu lilipoasisiwa mwaka 2009, Simba itasafiri hadi Tanga kwa ajili ya mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Singida Fountain Gate itakayopigwa Agosti 10 kisha kuigeukia Ligi Kuu Bara itakayoanza Agosti 15.

Ikiwa kambini Simba imecheza mechi tatu za kirafiki za kujipima ngumu, ikitoka sare ya 1-1 na Zira Fc kisha kuifunga Turan PFK 2-0 katika mchezo wa kwanza na kupoteza 1-0 na wapinzani hao hao juzi jioni, huku baadhi ya nyota wa timu hiyo na kocha Roberto Oliveira ‘Robertinho’ wakitamba.

Tuanze na kocha. Akizungumza na gazeti hili, kocha Robertinho alisema amefurahishwa na maendeleo ya timu yake kuanzia mchezaji mmoja mmoja hadi kikosi kizima na sasa anaweza kuthubutu kusema ‘sasa waleteni’, kwa madai timu hiyo ipo tayari kuanza msimu.

Kocha huyo Mbrazil alisema usajili uliofanywa kwa msimu huu umekuwa chanya katika kikosi chake na wachezaji waliosajiliwa wengi wana viwango vya juu na wameingia kwa haraka kwenye mifumo yake aliyoifundisha huko Uturuki.

“Kwa sasa tupo tayari kwa mashindano, nawapongeza wasaidizi wangu, tumefanya kazi kubwa kuhakikisha wachezaji wetu wanakuwa timamu kimwili, kiakili na kimbinu jambo ambalo ni muhimu sana kwetu,” alisema Robertinho na kuongeza;

“Haikuwa kazi rahisi, bali utayari wa kila mmoja, hata wale wachezaji wapya walioingia, wamefiti haraka kwenye mifumo na mbinu zetu, ni kitu kizuri kwetu na tunatarajia kuwa na msimu bora zaidi pale mashindano yatakapoanza.”

SOMA NA HII  KISA KUWA KUNDI MOJA NA SIMBA...VIPERS WAJIHAKIKISHIA USHINDI NYUMBANI NA UGENINI..

1 COMMENT