Home Yanga SC YANGA: TUMEJIANDAA NA MCHEZO WETU DHIDI YA RUVU SHOOTING

YANGA: TUMEJIANDAA NA MCHEZO WETU DHIDI YA RUVU SHOOTING


KOCHA wa Makipa wa Klabu ya Yanga, Razack Siwa amesema kuwa wana imani ya kupata matokeo chanya kwenye mchezo wa kesho dhidi ya Ruvu Shooting unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.

Siwa amesema kuwa maandalizi yapo vizuri na wana imani ya kupatapointi tatu mbele ya Ruvu Shooting.

“Tumejianda vizuri na mchezo wetu wa kesho dhidi ya Ruvu Shooting, pia nafikiri haya mapumziko tuliyoyapata yametusaidia sana kutengeneza timu na tupo tayari kwa mchezo.

“Wachezaji wote wapo vizuri na hakuna ambaye hayupo tayari ni suala la kusubiri na kuona namna ambavyo hali zao zitakuwa kwani kila kitu kipo sawa,” amesema.

Kwenye msimamo Ruvu Shooting ipo nafasi ya 10 na pointi 37 inakutana na Yanga iliyo nafasi ya pili na pointi 61.

SOMA NA HII  HII HAPA SIKU YA SIMBA, YANGA KUJUA 'VIBONDE' WAO WA ROBO FAINAL CAF...