Home epl RATIBA YA LIGI KUU ENGLAND YAWEKWA WAZI, CITY KUANZIA UGENINI

RATIBA YA LIGI KUU ENGLAND YAWEKWA WAZI, CITY KUANZIA UGENINI


 CHAMA cha Soka England (FA), kimetangaza ratiba ya Premier League kwa msimu wa 2021/22 ambapo tayari kila timu zishajua namna mambo yatakavyokuwa.

Msimu ujao mechi zinatarajiwa kuaza kuchezwa Agosti 14, 2021.


Katika ratiba hiyo, mabingwa watetezi, Manchester City watakuwa wageni wa Tottenham, mchezo unaotarajiwa kuwa mkali kutokana na ukubwa wa timu hizo.

Wageni ndani ya ligi hiyo, Brentford watawaalika Arsenal, huku Norwich nao wakiwa wenyeji wa Liverpool na Watford dhidi ya Aston Villa.

Mechi zingine ni; Burnley v Brighton, Chelsea v Crystal Palace, Everton v Southampton, Leicester v Wolves, Man Utd v Leeds na Newcastle v West Ham.

SOMA NA HII  ULAYA NI ULAYA TU....WAFANYAKAZI REAL MADRID WAPEWA NDINGA MPYAA...GARI MOJA BIL 3...