Home Habari za michezo AL AHLY ATAKUBALI KUENDELEZA UTEJA DHIDI YA SIMBA LEO AFL

AL AHLY ATAKUBALI KUENDELEZA UTEJA DHIDI YA SIMBA LEO AFL

Habari za Simba

Leo dunia ya soka itahamia Tanzania katika Uwanja wa Benjamin Mkapa. Ni katika uzinduzi wa michuano mipya ya African Football League ambapo pamoja na shamrashamra za ufunguzi wake, kutapigwa mechi ya kiume kati ya Simba na Al Ahly kutoka Misri.

Simba imekuwa timu tishio kwa siku za hivi karibuni, ikiwa imefanya makubwa kwenye soka la Afrika, iliitangaza kuwa timu ya saba kwa ubora baada ya kufika robo fainali mara tatu mfululizo ya Ligi ya Mabingwa na mara moja Kombe la Shrikisho.

Simba wamekuwa bora wanapocheza na Ahly Kwa Mkapa, wakiwa wamekutana nao mara nne na kupata ushindi wa asilimia 100, yaani walishinda michezo yote na huu utakuwa mchezo wa tano wanakutana.

SOMA NA HII  SALIM ALLY AISHIKA PABAYA SIMBA..... ISHU IKO HIVI