Home Azam FC UKIACHANA NA KIPUTE CHA SIMBE LEO….YANGA WAINGIA MTEGO WA AZAM FC….

UKIACHANA NA KIPUTE CHA SIMBE LEO….YANGA WAINGIA MTEGO WA AZAM FC….

Azam vs Yanga

DERBY ya kibabe inatarajiwa kuunguruma Jumatatu katika Uwanja wa Azam Complex Chamazi Jijini Dar es Salaam ikiwa na vita ya kukaa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Bara.

Mtanange huo wa kukata na shoka Yanga ndiye mwenyeji ambaye anatumia uwanja wa nyumbani wa mpinzani wake, Azam.

Mashabiki wa soka masikio yao ni katika dakika 90 za mchezo huo kutokana na rekodi iliyonayo Yanga kwa Azam FC.

Vita hiyo endapo Yanga ikishinda mchezo huo itaongoza ligi kwa pointi 15, ikiwazidi watani zao Simba wenye pointi kama hizo, lakini ikiwa na mabao mengi (15) ikiruhusu mawili pekee wakati Simba ikifunga mabao 14 na kuruhusu manne.

Azam inatakiwa kushinda mchezo huo ikizingatia iko nyumbani na endapo itavuna pointi tatu itaishusha Simba kileleni kwa kufikisha pointi 16. Endapo Yanga itatoka sare itakuwa na pointi 13 ambazo hazitaivusha huku Azam itakuwa na pointi 14 zitakazoifanya ishindwe kukaa kileleni mbele ya Simba.

Ili kuiondoa Simba katika nafasi hiyo wababe hao wanatakiwa kushinda mchezo huo na endapo itakwama, basi vita hiyo itakosa mshindi.

Mbali na vita ya kukaa kileleni mwa msimamo lakini pia mchezo huo utawakutanisha ndugu wa zamani, Yannick Bangala ambaye hakubahatika kucheza mchezo uliopita wa Ngao ya Jamii ulioikutanisha miamba hiyo jijini Tanga huku Feisal Slaum ‘Fei Toto’ akisubiriwa kwa hamu.

Mchezo wa Ngao ya Jamii, Fei alishindwa kufurukuta kuonyesha kiwango chake ambacho wengi wanakijua na hiyo huenda ilichagizwa na hofu na kupania mchezo. Wengi wanatamani kuuona ubora wa nyota huyo aliyejiunga akitokea Yanga lakini huku makazi mapya anaonekana kupoa wakati matumaini makubwa yako miguuni mwake kwa kushirikiana na wenzake.

Michezo ya hivi karibuni ambayo timu hizo zimekutana ni wa Ngao ya jamii ambao Yanga ilishinda mabao 2-0 huku msimu wa 2021/22 Yanga ilishinda 2-0 raundi ya kwanza na ya pili Azam ilipoteza mabao 2-1.

Msimu uliopita raundi ya kwanza timu hizo zilitoshana nguvu kwa kutoka sare ya kufungana mabao 2-2 na raundi ya pili Azam ilichezea kichapo cha mabao 2-3.

SOMA NA HII  BAADA YA KUONA VIWANGO VYA MASTAA WAPYA SIMBA...MBRAZILI KAGUNA WEE..KISHA AKASEMA HILI...