Home Simba SC SIMBA SC WAFANYA KWELI SUDANI..!!

SIMBA SC WAFANYA KWELI SUDANI..!!

 


Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika, Wekundu wa Msimbazi Simba SC, wamelazimishana sare ‘tasa’ dhdi ya yimu ya Al Merrikh ya Sudani katika mchezo uliomalizika jioni ya leo katika dimba la Al Hilal Stadium nchini Sudani.

Katika mchezo ambao ulikuwa wa kasi na vuta ni kuvute kwa pande zote mbili, umeshudiwa Simba SC wakitawala mchezo huo kwa kiasi kikubwa huku wachezaji wake wa eneo la ushambuliaji wakikosa umakini katika kumalizia nafasi zilizotengenezwa na viungo wa timu hio.

Kwa matokeo haya, Simba SC inakuwa imejikusanyia jumla ya alama 7 wakiwa kileleni katika kundi lao.

Taarifa zinasema kuwa Simba SC wataanza safari ya kurudi Tanzania mapema hii leo kuja kujiandaa na mchezo wa marudiano dhidi ya mabingwa hao wa Sudani, klabu ya Al Marrikh katika mchezo utakaochezwa wikiendi ijayo katika dimba la Mkapa.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI NA YANGA KESHO KUTWA....KOCHA SIMBA AINGIA UBARIDI..ADAI LAZIMA JAMBO LITOKEE SIKU HIYO...