Home Yanga SC FEI TOTO AREJESHA MATUMAINI YANGA

FEI TOTO AREJESHA MATUMAINI YANGA


 NYOTA wa kikosi cha Yanga, Feisal Salum, ‘Fei Toto’ kwa sasa anaendelea vema baada ya kupata maumivu kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya KMC.

Mchezo huo ulicohezwa Uwanja wa Mkapa, vinara hao wa ligi wenye pointi 57 baada ya kucheza jumla ya mechi 26 waligawana pointi mojomoja kwa kuwa ubao ulisoma Yanga 1-1 KMC.

Nyota huyo chini ya Kaimu Kocha Mkuu, Juma Mwambusi alikosekana kwenye mechi mbili ilikuwa dhidi Yanga 1-0 Biashara United na mbele ya Gwambina FC ubao ulisoma Yanga 1-0 Gwambina.

Kwa mujibu wa Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh amesema kuwa nyota huyo anaendelea salama.

“Fei Toto kwa sasa yupo vizuri na anaendelea na program za mwalimu ili kurejea kwenye ubora wake, kikubwa mashabiki wazidi kutuombea ili tufanye vizuri kwenye mechi zetu zijazo,” amesema.

Yanga kwa sasa inaendelea na maandalizi kwa ajili ya mchezo wao wa ligi dhidi ya Azam FC unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Aprili 25.

Mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Azam Complex, ubao ulisoma Azam FC 0-1 Yanga.

Kurejea kwa kiungo huyo kunarejesha matumaini ya vinara hao kuongeza viungo eneo la kati kwa ajili ya kuendelea kupambania taji la ligi.

SOMA NA HII  BAADA YA KUKABIDHIWA RUNGU LA USAJILI....NABI APIGA 'STOP' ...AMKINGIA KIFUA MCHEZAJI WAKE...