Home Uncategorized KIUNGO ANAYEWINDWA NA SIMBA ATOA LA MOYONI

KIUNGO ANAYEWINDWA NA SIMBA ATOA LA MOYONI

BARAKA Majogoro, kiungo mwenye rasta kichwani anayekipiga Polisi Tanzania inaelezwa kuwa anawindwa na Simba amesema kuwa neno kubwa kwa watanzania ni kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona.
 Majogoro alisema kuwa masuala ya kujiunga na timu kubwa ambazo ni Simba na Yanga yapo kila siku ila cha kwanza lazima tahadhari ichukuliwe.
“Nimekuwa nikiskia habari nyingi kuhusu mimi ila kwanza ninapenda kuwaambia watanzania kwa sasa ni muhimu kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona.
“Ninaweza kusema kwamba ninakwenda Simba ama Yanga ila kikubwa ni afya yangu kwanza na hao mashabiki hivyo ninapenda kuwaomba wasipuuzie taarifa zinazotolewa na Wizara ya afya pamoja na Serikali,” alisema Majogoro.
Polisi Tanzania ipo nafasi ya sita kwenye msimamo ikiwa imecheza mechi 29 kibindoni ina pointi 45. 
SOMA NA HII  SIMBA KUIFUATA LEO STAND UNITED SHINYANGA