Home kimataifa SADIO MANE ATAJA MABAO ANAYOTAKA KUFUNGA

SADIO MANE ATAJA MABAO ANAYOTAKA KUFUNGA


 SADIO Mane, mshambuliaji wa Liverpool raia wa Senegal ambayo ipo ndani ya bara la Afrika amesema kuwa anataka kutupia jumla ya mabao 30 ndani ya kikosi hicho kwa msimu wa 2021/22.

Nyota huyo ni moja ya washambuliaji makini na wenye juhudi ndani ya uwanja ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu wa Liverpool, Jurgen Klopp.

Mane mwenye miaka 29 amekuwa akijitolea kwa ajili ya jamii yake nchini Senegal amesema kuwa haikuwa mpango wake kuyeyusha msimu uliopita na mabao 16 jambo ambalo limempa hasira ya kupambana.

Amejiunga na timu hiyo ya Liverpool inayoshiriki Ligi Kuu England msimu wa 2016 ametupia jumla ya mabao 98 katika michezo 48. Yupo na mshikaji wake Mohamed Salah raia wa Misri.

Mane amesema:”Nataka kuona nafunga mabao zaidi ya 30 ikiwezekana sana kwa msimu huu pia na kuwatengenezea nafasi wengine kwa ajili ya kufunga,” .

SOMA NA HII  TOTTENHAM WAJIPANGA KUMPATA MRITHI WA HUGO