Home news YANGA YATUMIA MUDA KUWASOMA WAPINZANI WAO, KAZI INAENDELEA

YANGA YATUMIA MUDA KUWASOMA WAPINZANI WAO, KAZI INAENDELEA


KUELEKEA kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika ambao ni wa hatua ya awali kati ya Yanga v Rivers United unaotarajiwa kuchezwa Jumapili, Septemba 12 Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi amekuwa akiwasoma wapinzani wao mara kwa mara.

Imeelezwa kuwa Nabi ambaye ni mkuu kwenye kitengo cha benchi la ufundi Yanga amekuwa akiwafuatilia wapinzani wake ili aweze kujua mbinu za kupata ushindi.

Habari kutoka ndani ya Yanga zimeeleza kuwa kocha huyo aliomba video mbili za mechi za Wanaijeria hao ambazo ni sawa na dakika 180 ambazo wapinzani wao walicheza hivi karibuni.

“Kocha amekuwa na utaratibu wa kuwaangalia wapinzani siku moja hadi siku mbili kabla ya mchezo husika tutakaokutana nao wikiendi.

“Amekuwa akiwaangalia wapinzani wake kwa kutumia video za mechi mbili hadi tatu na lengo la kuangalia ni kuweza kujua ubora na upungufu wao ulipo,” .

Mkuu wa kitengo cha Habari, Mawasiliano cha Yanga, Hassan Bumbuli amesema:”Tayari tumekamilisha mahitaji yote ya mwalimu ambayo ameyataka, kazi tumuachie yeye na wachezaji wake kuhakikisha tunapata ushindi,” .

Tayari kikosi hicho kinaendelea na mazoezi kwa ajili ya mechi hiyo inayotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Yupo mtambo wao wa mabao msimu uliopita ambaye ni Yacouba Songne na alitupia mabao 8 pia Ramadhan Kabwili naye yupo pamoja na Said Ntibanzokiza naye ni miongoni mwa wachezaji ambao wapo kambini, kijiji cha Avic.

SOMA NA HII  YANGA WAANZA MBINU ZA BAYERN..WAPEWA SEKUNDE 5.. PABLO ADUWAZA MASTAA SIMBA...