Home Habari za michezo KUHUSU ISHU YA MIQUISSONE NA SIMBA…’UPDATE’ MPYA HIZI HAPA KUTOKA AL AHLY...

KUHUSU ISHU YA MIQUISSONE NA SIMBA…’UPDATE’ MPYA HIZI HAPA KUTOKA AL AHLY YA MISRI…

Tetesi za usajili Simba

Inaelezwa kuwa uongozi wa Simba SC na Al Ahly ya Misri, umefikia makubaliano ya kumsajili kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Luis Miquissone raia wa Msumbiji kwa mkataba wa mkopo, huku wakiwa tayari kumuuza kiungo wao, Msenegali, Pape Sakho kuelekea nchini Ufaransa.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally, amesema: “Usajili unaendelea, bado mchezaji mmoja na viongozi wa Simba SC wasikivu sana, sasa ni zamu ya Mmakonde (Luis Miquissone) usajili wanaousubiri sana Wanasimba kuuona kwa sasa.”

Simba SC imekuwa ikipambana kumrudisha Miquissone ambaye tangu imuuze kwenda Al Ahly, amekuwa na wakati mgumu wa kupata nafasi kiasi cha kupelekwa kwa mkopo klabu ya Abha ya nchini Saudi Arabia ambayo tayari imemrudisha.

Awali, Simba ilienda Al Ahly kumuomba mchezaji huyo kwa mkopo ambao utakuwa na makubaliano ya kulipa mshahara wa shilingi milioni 25, huku timu yake imlipe mshahara wa shilingi milioni 55, kitendo ambacho kiligomewa na timu hiyo kabla ya Simba kukaa upya na mshambuliaji huyo kukamilisha suala hilo.

Taarifa za uhakika kutoka ndani ya uongozi wa Simba SC, umesema kuwa, Miquissone na Simba SC wamefikia makubaliano mazuri ya kumsaini kwa mkopo ambao utakuwa na mshahara waliokubaliana kabla ya kwenda kumalizana na Al Ahly, huku Simba SC wakiwa wamepanga kutumia nafasi hiyo kuziba pengo la Sakho anayetarajia kuuzwa Ufaransa.

“Ni kweli suala la Miquissone sasa huenda likawa limeisha kwa sababu mchezaji mwenyewe na uongozi wamshamalizana kila kitu, kilichobaki ni mazungumzo kati ya Al Ahly ili kuona wanaweza vipi kukamilisha usajili huo wa mkopo kabla ya kuanza kwa msimu upya.

“Ujio wa Miquissone uongozi unaamini utasaidia kurudisha makali ya timu na ikizingatiwa wamepanga kumuuza Sakho, hivyo itakuwa sehemu ya moja ya kuziba nafasi yake, Sakho anaweza kwenda Ufaransa ingawa bado wanaficha upande wa timu mpaka sasa,” amesema mtoa taarifa.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally, amehitimisha kwa kusema: “Simba SC kuna Mmakonde mmoja (mimi) sasa bado Mmakonde mwingine kutua ndani ya kikosi cha Simba. Vuta picha kikosini yupo Aubin (Kramo), Willy Essomba Onana, Jean Baleke, halafu kuna Miquissone.”

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI NA WAGHANA....MASTAA YANGA WAAPA 'KUFA NA MTU' UWANJANI....