Home Uncategorized HIKI NDICHO KINACHOITESA KAGERA SUGAR KWA SASA NDANI YA LIGI

HIKI NDICHO KINACHOITESA KAGERA SUGAR KWA SASA NDANI YA LIGI



KOCHA Mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Maxime amesema kuwa matokeo wanayoyapata kwenye ligi yanatokana na ushindani kuwa mkubwa wanajipanga kwa sasa kurejea kwenye ubora wao.


Kagera Sugar, jana ilipoteza mbele ya Polisi Tanzania kwa kufungwa mabao 2-1 uwanja wa  Ushirika, Moshi ikiwa imetoka kufungwa Coastal Union bao 1-0 uwanja wa Mkwakwani.

Maxime amesema :”Ligi ni ngumu na kila timu inapambana kupata matokeo chanya, hatuna mashaka na uwezo wa wachezaji makosa yetu tutayafanyia kazi,” amesema.

Mchezo wa ligi unaofuata kwa Kagera Sugar ni dhidi ya Yanga utachezwa Januari 15 uwanja wa Uhuru.
SOMA NA HII  MOHAMED SALAH AMPASUA KICHWA JURGEN KLOPP KISA KUKOSEKANA KWAKE MIEZI MINNE