Home Habari za michezo ISHU YA SIMBA NA MGUNGA BADO PASUA KICHWA…MWENYEWE AWAWEKEA NGUMU MABOSI…

ISHU YA SIMBA NA MGUNGA BADO PASUA KICHWA…MWENYEWE AWAWEKEA NGUMU MABOSI…

Kocha Msaidizi Simba SC

HUKO Simba hali sio shwari kwa aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Juma Mgunda baada ya kuonekana akiwa na kikosi cha vijana.

Mgunda ameshuhudiwa akiwa kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo Mbweni wakati wa kutafuta vipaji vitakavyojiunga na timu hiyo chini ya kocha mkuu, Selemani Matola na mkuu wa programu za soka la vijana, Patrick Rweyemamu.

Mgunda ambaye hakusafiri na Simba kwenda nchini Uturuki kwa ajili ya maandalizi ya msimu, amekuwa kwenye sintofahamu kubwa kuhusiana na hatima yake ndani ya timu hiyo inayonolewa na Mbarazili, Roberto Oliveira ‘Robertinho’.

Taarifa za mwanzo zipo  zinaeleza Mgunda alitakiwa kupewa timu ya Simba Queens jambo ambalo hata hivyo yeye mwenyewe ilielezwa hayuko tayari kufundisha kwa upande huo kwenye soka la wanawake.

Kuonekana kwa Mgunda kwenye soka la vijana kunaibua maswali mengine ingawa hata hivyo viongozi wa Simba bado hawajaweka wazi cheo chake kipya.

Mgunda alijiunga na Simba Septemba 7, mwaka jana akitokea Coastal Union baada ya timu hiyo kuachana na Zoran Maki aliyesitishwa mkataba wake.

SOMA NA HII  SHIBOUB AANZA KUKIWASHA NA SIMBA ZANZIBAR...PABLO AMWEKA KWENYE 'LISTI'...HUYO MUAIVORY MHH...