Home Uncategorized ISHU YA BEKI WA COASTAL UNION KUIBUKIA SIMBA IPO NAMNA HII

ISHU YA BEKI WA COASTAL UNION KUIBUKIA SIMBA IPO NAMNA HII

BAKARI Mwamnyeto, nahodha wa Coastal Union amesema kuwa hana hiyana iwapo kikosi cha Simba kitahitaji saini yake.

 Inaelezwa kuwa mabosi wa Simba wanahitaji huduma ya  beki huyo hali iliyofanya kumtengea dau la milioni 85.
Safu yake ya ulinzi imejijengea ukuta makini ambapo inashika nafasi ya pili kwa kuruhusu mabao machache ikiwa imefungwa 19 msimu huu na kinara akiwa ni Simba ambaye amefungwa mabao 15.
Beki huyo amesema:”Mimi ni mchezaji siwezi kuchagua timu ila kikubwa ni makubaliano na maslahi iwapo kila kitu kitakuwa sawa ninaweza kutumika ndani ya Simba hata nje ya Simba kwangu fresh,”.
SOMA NA HII  MWADUI FC: TUPO TAYARI KUSAKA POINTI TATU ZA SIMBA