Home Habari za michezo MKUDE HUYOOO TAIFA STARS

MKUDE HUYOOO TAIFA STARS

Mkude atambulishwa yanga

Kiungo wa Yanga SC, Jonas Mkude ameitwa katika kikosi cha timu ya taifa Tanzania (Taifa Stars) kwa ajili ya mchezo wa kutafuta nafasi ya kufuzu AFCON dhidi ya Algeria.

Mkude aliyejiunga na Yanga SC hivi karibuni katika dirisha hili akitokea Simba SC atakuwa sehemu ya kikosi cha Stars kitakachokwenda kupambana na Algeria ugenini, Septemba 7.

Stars inahitaji alama moja katika mchezo huo ili iweze kufuzu fainali hizo ambazo mara ya mwisho ilifuzu mwaka 2019 nchini Misri.

SOMA NA HII  HAWA HAPA NDIO WAPINZANI WA SIMBA,YANGA KIMATAIFA