Home Habari za michezo HIVI NDIVYO SVEN ALIVYOIZIDI UJANJA SIMBA KWENYE DILI LA MIQUISSONE…LABDA WAJARIBU MSIMU...

HIVI NDIVYO SVEN ALIVYOIZIDI UJANJA SIMBA KWENYE DILI LA MIQUISSONE…LABDA WAJARIBU MSIMU UJAO…


Aliyekuwa mchezaji wa zamani wa klabu ya Simba SC na sasa akiwa ni mchezaji wa Al Ahly ya nchini Misri, Luis Miquissone atajiunga na klabu ya Abha ya Saudi Arabia kwa mkopo wa msimu mzima.

Miquissone mwenye umri wa miaka 27 atajiunga na klabu hiyo baada ya timu yake ya Ahly kupokea ofa ya USD 300,000 kutoka katika klabu hiyo yenye maskani yake Saudi Arabia.

Miquissone alinunuliwa na Simba kutoka UD Songo ya Msumbiji na kupata mafanikio mengi akiwa na Simba hasa kufanya vizuri kwenye michuano ya CAF kulifanya avutie kwenye vilabu vingi barani Africa.

Ni misimu miwili tuu ambayo ametumikia kwa mabingwa mara nyingi wa kombe la klabu bingwa Afrika baada ya kutopata nafasi ya mara kwa mara kunako klabuni hapo, na sasa anaenda kutafuta changamoto mpya Uarabuni.

Al Ahly ambayo walimtupia virago kocha wao waliyepata nae mafanikio makubwa Pitso Mosimane, na ndio alimsajili Miquissone. Ni siku chache pia zimepita wamemtimua kocha wao mpya Mreno Ricardo Soares ambaye ameshindwa kutetea ubingwa ambao wameukosa tena mara hii. Kitendo hicho kimefanya asidumu klabuni hapo kwa muda na kupewa mkono wa kwaheri na klabu huyo.

Wakati kwa upande huo wapinzani wao Zamalek wamekuwa bora sana baada ya kubeba ubingwa mara mbili mfululizo. Mpaka sasa Abha imecheza mechi mbili imeshinda moja na imepoteza moja ipo nafasi ya 10.

SOMA NA HII  AHMED ALLY: BAADA YA KUPIGWA NA RAJA...SIMBA NZIMA TULIKATA MOTO...HATUWAWEZZI WALE..