Home Habari za michezo AHMED ALLY: BAADA YA KUPIGWA NA RAJA…SIMBA NZIMA TULIKATA MOTO…HATUWAWEZZI WALE..

AHMED ALLY: BAADA YA KUPIGWA NA RAJA…SIMBA NZIMA TULIKATA MOTO…HATUWAWEZZI WALE..

Simba vs Raja

Afisa Habari wa Simba SC, Ahmed Ally amesema, kwenye mechi yao ya pili ya Hatua ya Makundi ya Klabu Bingwa walikata moto baada ya kufungwa goli la tatu na Raja Casablanca.

Ahmed alisema, siku hiyo alikuwa hafatilii mechi bali zaidi alikuwa akiangalia jinsi ambavyo mashabiki wanashangilia kabla na hata baada ya kufungwa.

“Ukweli ni kwamba Raja hatuwawezi kwa kushangilia lakini siku ile walibebwa zaidi na ushindi wao, laiti tungewafunga sisi, wale wangeloa lakini bahati mbaya walipotufunga wao ndipo na sisi tukakata moto hasa baada ya kufungwa goli la tatu,” alisema Ahmed.

Simba wanatarajia kuwakaribisha Vipers SC Marchi 7, 2023 kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar ikiwa ni mchezo wa marudiano baada ya wa awali kushinda 1-0 ugenini.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMAMOSI