Home Habari za michezo JULIO : WAAMUZI BONGO ‘WANAIKOSTI’ YANGA KIMATAIFA…VIONGOZI WAO WAACHE UJANJA UJANJA…

JULIO : WAAMUZI BONGO ‘WANAIKOSTI’ YANGA KIMATAIFA…VIONGOZI WAO WAACHE UJANJA UJANJA…

Habari za Michezo

Baada ya timu ya Yanga kutoka suluhu dhidi ya Club African kwenye mchezo wa kwanza wa kufuzu hatua ya makundi kwenye kombe la Shirikisho Afrika, CAF, mchezaji na kocha wa zamani wa Simba, Jamhuri Kiwelu Julio ameitaka timu hiyo kukubali kujiwekeza kwa muda mrefu ili kufanya vizuri kimataifa.

Akizungumza, Julio amesema kuwa, kila kitu kinahitaji maandalizi hivyo Yanga hawawezi kufanya usajili mara moja na kutarajia matokeo mazuri, jambo linalohitaji muda kama walivyofanya wenzao Simba.

“Maamuzi yanatukosti sana, leo Yanga wanakuwa bora kwenye ligi ya ndani kwa sababu ya kubebwa na waamuzi, wanatakiwa kuwekeza kimataifa,” alisema.

“Ukizungumzia Simba ipo kwenye kiwango kwa sababu imejiandaa kwa muda mrefu, Yanga wasitegemee ubingwa tu wa mwaka jana kumnunua Aziz Ki, Mayele tayari watakwenda kushindana kama Simba.

“Na si kwamba wachezaji hawa ni wabaya, bado hawajapata muunganiko na wachezaji waliokuwepo kwa kuwa ni wachezaji wapya hawajawajua sawasawa kina Fei wacheze nao vipi, ushindi wao unatokana na juhudi binafsi.

“Ki ukweli ukilinganisha Simba na Yanga katika Ligi ya ndani na mashindano ya kimataifa, Simba wapo vizuri zaidi kwa kuwa wamejiwekeza muda mrefu hata baadhi ya wachezaji wakiondoka na kuja wengine wanawahi kukopi mfumo na wanafanya vizuri.

“Yanga waache kuwapa presha wachezaji na badala yake viongozi wasajili timu kwelikweli na wakubali kukaa kwa muda mrefu kwa kujipanga ili mambo yaende,” alisema Julio.

SOMA NA HII  MOMO AWASHAURI VIONGOZI WA SIMBA, HERSI WA YANGA ATAJWA

1 COMMENT

  1. we mwandishi ni mwongo tena sana na nadhani mnapotosha ukweli,Yanga walifunga Zalan mkasema vibonde je wale ni wa nchi gani,halafu wametolewa na Al hilal mkasema hawawezi Kimataifa,je Big Bullet na De Agosto na ZALAN kuna tofauti gani matimu yote mabovu.