Home Uncategorized HIZI NDIZO SILAHA KUWA MBILI ZA WAPINZANI WA YANGA KIMATAIFA LEO

HIZI NDIZO SILAHA KUWA MBILI ZA WAPINZANI WA YANGA KIMATAIFA LEO


TOWNSHIP Rollers mabingwa wa Botswana leo watakuwa uwanja wa Taifa wakimenyana na Yanga mchezo wa awali wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Rollers walimaliza Ligi na point 68 na kubeba ubingwa msimu uliopita baada ya kushinda mechi 20 kati ya 30.

Waliambulia sare 8 walipotezamechi 2. Kawaida wana uwezo mkubwa wa kuuchezea mpira na wanaitumia kama silaha yao katika mambo mawili makuu.

Jambo la kwanza ni pasi ambazo wanazicheza kwa kasi ikiwa ni sehemu ya kujilinda kwa kuwa kama wana mpira ni uhakika hautawafunga.

Jambo la pili wanapokuwa na mpira mara kadhaa wanakuwa wanaangalia kama kuna nafasi ya kupenya na kufunga mapema.

SOMA NA HII  VIDEO:MWENYEKITI WA ZAMANI WA SIMBA ADEN RAGE ASIMULIA ALIVYOKAMATWA NA TAKUKURU

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here