Home Uncategorized TANZIA: MKE WA NAHODHA WA AZAM FC AGREY MORIS ATANGULIA MBELE ZA...

TANZIA: MKE WA NAHODHA WA AZAM FC AGREY MORIS ATANGULIA MBELE ZA HAKI


TAARIFA ya Tanzania kutoka kwa Uongozi wa Azam FC leo ipo namna hii:-

Azam FC tumepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha mke wa Nahodha wetu, Agrey Moris, aliyefariki dunia jana jioni wakati akiwa kwenye harakati za kujifungua.

Tunatoa salamu zetu za pole kwenda kwa familia ya Moris, pamoja na ndugu, jamaa na marafiki na wote walioguswa na msiba huo.

Azam FC tunaungana na familia ya marehemu na tunamuomba Mwenyezi Mungu, awajalie nguvu na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu.

Bwana ametoa na Bwana Ametwaa, Jina lake lihimidiwe. Amen.

SOMA NA HII  MFUMO MPYA WA SIMBA SASA KIBOKO,PUNGUZO KWA TIKETI MPAKA ASILIMIA KUMI