Home Habari za michezo MATOLA : NIMECHOKA KUGEUZWA KICHAKA CHA MATATIZO SIMBA….NINA NDOTO ZANGU NA MIMI…

MATOLA : NIMECHOKA KUGEUZWA KICHAKA CHA MATATIZO SIMBA….NINA NDOTO ZANGU NA MIMI…

Kocha Msaidizi wa Simba SC, Selemani Matola amekanusha taarifa ambazo zimekuwa zikitolewa na baadhi ya mashabiki kuwa anaihujumu timu yake hasa inapopata matokeo mabaya.

“Haiwezekani mashabiki wanigeuze mimi kichaka cha lawama tena wakati mwingine wananipa tuhuma za kuhujumu timu. Inawezekana vipi mimi nikahatarisha kibarua changu kwa kuhujumu kazi yangu!

“Mimi nina ndoto za kuwa Kocha Mkubwa Afrika, siwezi kuingia kwenye kashfa za kuhujumu kazi yangu ninayoitegemea” – Selemani Matola – Kocha Msaidizi Simba SC.

SOMA NA HII  KILA MCHEZAJI ATAPATA NAFASI YANGA, GAMONDI AFUNGUKA KILA KITU