Home Yanga SC STRAIKA YANGA AWAWASHIA MOTO MATAPELI

STRAIKA YANGA AWAWASHIA MOTO MATAPELI


MSHAMBULIAJI mpya wa Yanga, Fiston Abdoul Razak ameijia juu Kampuni ya uwakala ya Heritage Soccer Agency na kuwaita matapeli kutokana na kampuni hiyo kudai haikushirikishwa katika dili la staa huyo kujiunga na Yanga.

Katikati ya wiki hii ilisambaa barua iliyokuwa imewasilishwa katika Shirikisho la Soka la Kimataifa ‘FIFA’, na Shirikisho la Soka Afrika ‘CAF’ na Shirikisho la Soka Tanzania ‘TFF’ ikidai mshambuliaji huyo amekiuka mkataba na kusaini Yanga bila ridhaa yao kama wasimamizi wake. 

Akizungumzia madai hayo Fiston amesema: “Hao jamaa ni matapeli, hiyo barua nimeiona, nikawapigia simu, nikawatukana na nimewaambia huo mnaofanya ni utapeli na kama wanawafanyia wachezaji wengine huko mtakuwa hamuwatendei  haki hata kidogo.

“Huwa sipendi ujinga na kitu wanachokifanya siyo sahihi kabisa kwa sababu sijawahi kufanya nao kazi, hawajawahi kunipa dili yoyote hata ya majaribio kwa nini waseme hivyo.

“Na ukiangalia hiyo barua yao imekatwa kwa chini, nafanya kazi na wakala watatu ambao ni raia wa Misri ila siyo wao maana hao wanaodai hivyo mmoja ni Mtanzania na tulishagombana,” 

SOMA NA HII  KAZE :- KUANZIA SASA LAZIMA TUONYESHANE MAKALI KWANZA..ILI TUHESHIMIANE