Home Uncategorized TAMBWE AIKOSOA SAFU YA ULINZI SIMBA, ATUMA OMBI KWA MBELGIJI

TAMBWE AIKOSOA SAFU YA ULINZI SIMBA, ATUMA OMBI KWA MBELGIJI


Straika wa Yanga kutoka Burundi, Amis Tambwe, amefunguka kwa kusema kuwa amefurahishwa na nafasi ya ushambuliaji ya Simba kufuatia ushindi waliopata katika mechi ya Ngao ya Jamii kwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-2.


Tambwe ambaye aliwahi pia kuichezea Simba miaka kadhaa iliyopita, amesema Simba wameimarika zaidi kunako eneo la ushambuliaji jambo ambalo limemfanya afunguke na kutoa pongezi hizo.

Katika mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ulishuhudiwa mabao yakiwekwa kimiani na Sharaf Shiboub aliyeingia kambani mara mbili sambamba na Clatous Chama aliyefunga moja huku Francis Kahata naye akifunga moja.

“Kusema ukweli safu ya ushambuliaji ya Simba imekuwa vizuri hivi sasa tofauti na msimu uliopita.

“Kusajiliwa kwa Deo Kanda na Kahata kumezidi kutia morali na makali mbele na uwepo wa Shiboub umesaidia kuwasaidia washambuliaji wanaofanya kazi ya kufunga”, amesema.

Mbali na kusifia, Tambwe pia amefunguka kwa kuikosa nafasi ya ulinzi akisema bado ina mapungufu.

“Kwenye safu ya ushambuliaji bado kuna matatizo yaleyale ambayo yaliigharimu timu msimu uliopita haswa kwa mechi za nyumbani na ugenini.

“Kwa maana hiyo wakikutana na washambuliaji wazuri wanaojua zaidi itakuwa ngumu kwao kuwazuia na makosa ya msimu uliopita yatazidi kujitokeza.

“Namuomba Kocha alifanyie kazi suala hilo ili kuhakikisha Simba inakuwa fiti kila idara”.
SOMA NA HII  EYMAEL ATAJA KITAKACHOIPA MATAJI YANGA, SVEN ALIUONA UBINGWA WA SIMBA