Home Habari za michezo HUU HAPA UKWELI KUHUSU KIFO CHA DK GEMBE…ALIKUWA TIMU KUBWA YA SIMBA...

HUU HAPA UKWELI KUHUSU KIFO CHA DK GEMBE…ALIKUWA TIMU KUBWA YA SIMBA AKASHUSHWA MPAKA TIMU YA WATOTO…


Simba SC leo Septemba 02, 2022 wamepata pigo kwa kuondokewa na aliyekuwa daktari wao, Yassin Gembe.

Simba wametoa taarifa ya kifo cha daktari wao kupitia ukurasa rasmi wa Instagram wakieleza kuwa amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu.

“Kwa masikitiko makubwa tunatangaza kifo cha aliyekuwa daktari wa timu yetu ya wanaume (Senior Team) ambaye kwasasa alikuwa daktari wa timu ya vijana (Youth Team), Dkt. Yassin Gembe ambacho kimetokea leo mchana kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.”

Simba wamesema taarifa zaidi kuhusu msiba huo watazitoa baadaye.

SOMA NA HII  CHAMA AWACHAMBUA WACHAMBUZI WA SOKA...MFUNGAJI BORA WA MUDA WOTE CAF