Home Habari za michezo BAADA YA KUONA NA ‘KUINJOYI’ FUNGATE…SAIDO AIPIGA MKWARA WA KUFA MTU AZAM...

BAADA YA KUONA NA ‘KUINJOYI’ FUNGATE…SAIDO AIPIGA MKWARA WA KUFA MTU AZAM FC…


YANGA inajiandaa na pambano lao dhidi ya Azam, huku kikosi chake kikizidi kuimarika kutokana na baadhi ya wachezaji waliokuwa majeruhi kurejea akiwamo Saido Ntibazonkiza aliyepo Burundi aliyepiga mkwara mapema.

Mbali na Saido, wengine waliokuwa majeruhi na kurejea uwanjani ni mabeki Yassin Mustafa, Kibwana Shomari, David Bryson na winga Jesus Moloko wanaojifua kwa sasa gym ya viwanja vya Gymkana kujifua kabla ya kuja kuliamsha katika ligi.

Taarifa njema kwa mashabiki wa na Yanga na kocha Nassredine Nabi aliyeko mapumziko mafupi Ubelgiji ni kupona kwa Saido ambaye msimu huu amehusika katika mabao 11 ya Yanga, akifunga sita na kuasisti mara tano huku pacha yake na mshambuliaji Fiston Mayele mwenye bao 10 ikiwa ya kuotea mbali.

Saido aliumia mguu Februari 27, kwenye mechi ya ligi dhidi ya Kagera Sugar, vinara hao wakishinda mabao 3-0, yeye kufunga bao la tatu la mchezo huo na baada ya hapo alikaa nje kwa matibabu kabla ya kutimkia nchini Bujumbura, Burundi kufunga ndoa na mkewe Samantha Uwera (Samira).

Mwamba huyo hakutaka kulaza damu kwani baada ya kufunga pingu za maisha Machi 19, alianza kufanya mazoezi mdogo mdogo katika Gym moja ya kifahari iliyopo Bujumbura, Burundi huku akifuata programu za madaktari wa Yanga alizopewa na baada ya hapo alihamia ufukweni alikokuwa akipiga matizi ya kukimbia na kuruka koni.

Inafahamika kuwa Saido aliomba kupumzika kutoitwa timu ya taifa, ili apate muda mzuri wa kujiweka fiti na kocha mkuu wa timu ya taifa ya Burundi Jimmy Ndayizeye alimuelewa na kumuacha aendelee na mazoezi binafsi na juzi alienda kwa wataalamu wa misuli kufanyiwa masaji na kuona muendelezo wa mguu wake ambapo kwa asilimia kubwa yuko fiti.

Mwishoni mwa mwezi huu nyota huyo atarejea Bongo kujiunga na chama lake na kujifua kitimu kabla ya kuwavaa Azam FC, April 6, na kuendelea na mechi nyingine za ligi na zile za Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC).

SOMA NA HII  KUMBE MAXI ALITAKIWA KUTUA SIMBA NA SIO YANGA..... ISHU IKO HIVI

Akizungumza kuhusu ubingwa, Saido alisema kwa msimu huu anaiona Yanga ikiwa na nafasi kubwa ya kubeba ubingwa huo kwani ina wachezaji wenye viwango bora, pia wanajituma kuhakikisha lengo lao linatimia.

“Msimu huu ni tofauti na misimu iliyopita, kama unavyoona timu imeimarika kutokana na usajili mkubwa uliofanywa na kila mchezaji anapambana kuhakikisha tunapata matokeo kwenye kila mechi. Naamini kwa kushirikiana wote kuanzia mashabiki, viongozi, benchi la ufundi na wachezaji tutafanya hivyo msimu huu kwani tulianza vizuri na tupo katika nafasi nzuri ya kufanya hivyo,” alisema nyota huyo wa zamani wa Caen ys Ufaransa.

Hadi sasa Yanga haijapoteza mechi hata moja kwenye ligi ikiwa kileleni mwa msimamo na pointi 48 ilizovuna kwa kushinda mechi 15 na kupata sare tatu kati ya 18 ilizocheza huku ikiwa imebakiza mechi 12 kumaliza ligi msimu huu.