Home Azam FC RASMI..JAMES KOTEI KUKIPIGA CHAMAZI COMPLEX…ISHU NZIMA IKO HIVI AISEE….

RASMI..JAMES KOTEI KUKIPIGA CHAMAZI COMPLEX…ISHU NZIMA IKO HIVI AISEE….

 


Timu ya Azam FC itakuwa na mechi ya kirafiki dhidi ya DTB Jumanne Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

Kwa Azam, mechi hiyo ni sehemu ya maandalizi ya mchezo wao ujao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Yanga SC Aprili 6, mwaka huu hapo hapo Azam Complex.

Na kwa DTB ambayo James Kotei ‘Baba Paroko’ anaichezea wataitumia mechi hiyo kujipanga kwa michezo yake ijayo ya ligi ya kuwania kupanda Ligi Kuu, ijulikanayo kama Championship.

Ikumbukwe Yanga wao watakuwa na mechi ya kujipima pia Jumatano hapo hapo Chamazi dhidi ya Mafunzo ya Zanzibar.

SOMA NA HII  HITIMANA AVUNJA UKIMYA SIMBA ...AFUNGUKA NAMNA MAMBO YALIVYO KUELEKEA MECHI YA KESHO...