Home Uncategorized SIMBA YASHAURI NAMNA YA KUMALIZA SAKATA LA MORRISON

SIMBA YASHAURI NAMNA YA KUMALIZA SAKATA LA MORRISON

 

KUTOKANA na mvutano wa kesi ya Bernard Morrison kuhusu suala la mkataba wake uongozi wa Simba umetoa pendekezo la namna ya kufanikisha suala hilo kuisha kwa amani. 


Ofisa Habari wa Simba Haji Manara kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika namna hii:-


“Kama suala la Morrison limekuwa gumu kwa TFF, bas ipigwe game moja kati ya Simba na Yanga, atakayeshinda ndo amchukue Morrison, mbona simple tu(rahisi).”

Jana Agosti 10 kesi ya Morrison ilianza kuskilizwa na Kamati ya Hadhi ya Wachezaji makao makuu ya Shirikisho la Soka Tanzania,(TFF) suala kubwa likiwa ni mvutano wake na mkataba ambapo yeye anasema kuwa mkataba wake ni wa miezi sita huku Yanga wakieleza kuwa ana dili la miaka miwili.

Kinachoongeza uzito ni kwamba mchezaji inaelezwa amesaini dili la miaka miwili jambo linaloongeza uzito kwa kila mmoja kuvutia upande wake.

SOMA NA HII  SIMBA YAINGIA ANGA ZA TP MEZEMBE, KUCHOMOKA NA BEKI MMOJA