Home news HITIMANA AVUNJA UKIMYA SIMBA …AFUNGUKA NAMNA MAMBO YALIVYO KUELEKEA MECHI YA KESHO…

HITIMANA AVUNJA UKIMYA SIMBA …AFUNGUKA NAMNA MAMBO YALIVYO KUELEKEA MECHI YA KESHO…


KUWAHESHIMU wapinzani ni moja ya silaha ambayo Simba wataitumia katika mchezo wao wa mtoano wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Red Arrows ya Zambia utakaopigwa Jumapili katika uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam.

Simba imepata nafasi ya kushiriki kombe la Shirikisho Afrika baada ya kuondolewa katika Ligi ya Mabingwa na Jwaneng Galaxy ya Botswana kwa jumla ya mabao 3-3 baada ya mchezo wa ugenini kushinda 2-0 huku wakipoteza nyumbani kwa kufungwa mabao 3-1.

Kocha msaidizi wa kikosi hicho Hitimana Thierry alisema, kuwaheshimu wapinzani wao na kucheza kwa tahadhari ni moja ya dhana yao kufanya vizuri kwenye mchezo huo.

Alisema, hata wachezaji wameambiwa hilo ili kuepuka yaliyojitokeza katika Ligi ya Mabingwa baada ya nyota wao kujiamini zaidi na kujikuta wakitoa nafasi kwa wapinzani kuwaondoa licha ya wao kuwa wanatangulia.

“Hata katika maisha ukimuheshimu mpinzani wao unaenda nae sawa, hivyo hata sisi tunatakiwa kufanya hivyo, ili tuweze kufanya vizuri nyumbani kabla ya kwenda ugenini,”

“Mimi ninaimani sana na wachezaji wangu, hata hao Arrows tumewaangalia na bado tunaendelea kuwaangalia sio wabaya, ni timu nzuri sana, tunatakiwa kupambana na kutumia vyema dakika 90 za nyumbani,” alisema.

SOMA NA HII  YANGA YAIPITA SIMBA KWENYE KLABU ZENYE THAMANI AFRIKA MASHARIKI...AZAM FC BABA LAO...