Home Uncategorized YANGA YATAJA SABABU YA KUSHINDA LEO MBELE YA MBAO FC

YANGA YATAJA SABABU YA KUSHINDA LEO MBELE YA MBAO FC


LEO Uwanja wa Taifa Yanga itaikaribisha Mbao FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa majira ya saa 1:00 usiku.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa wachezaji wana morali kubwa ya kupata ushindi jambo litakalowapa nguvu ya kuendelea kujiweka kwenye nafasi nzuri.

Nugaz amesema: “Taratibu kikosi kinazidi kuimarika na kwa namna ambavyo tunapata ushindi inatupa nafasi nzuri ya kusonga mbele kwenye mechi zetu zinazofuata kikubwa mashabiki wajitokeze kutupa sapoti.

“Muda ni usiku na inatokana na kwamba leo ni siku ya kazi tunataka kutoa uhuru kwa mashabiki kuona namna Yanga ya Wananchi inavyofanya kazi ya kujituma,”.

SOMA NA HII  ISHU YA KIBALI CHA MORRISON SIMBA WAIJIBU YANGA KIMTINDO