Home Habari za michezo MTOTO WA NABI KUAMUA HATMA YA BABA’KE YANGA….ATUA BONGO KUSET MITAMBO…

MTOTO WA NABI KUAMUA HATMA YA BABA’KE YANGA….ATUA BONGO KUSET MITAMBO…

Habari za Yanga SC

Rais wa Yanga Injinia Hersi Said amevunja ukimya juu ya hatma ya kocha wao Nasreddine Nabi akisema kocha huyo bado ataendelea kubaki klabuni hapo.

Hersi ameyasema hayo wakati akihojiwa asubuhi hii na kituo cha Radio Cha Wasafi akisema Yanga bado inamuhitaji Nabi.

“Kila mkataba una kikomo nikweli mkataba wa Nabi unafikia tamati mwisho wa msimu huu na klabu ilishaanza hatua ya kumuongezea mkataba mwingine,”amesema Hersi.

Aidha Hersi ameongeza kuwa tayari Nabi ameshamleta nchini mwanaye Hedi Nabi ambaye ndio msimamizi wake wa masuala ya mkataba katika hatua za mwisho za kusaini mkataba mpya.

“Jana tumerejea nchini nadhani Maulid (Kitenge) ulikuwepo kwenye ndege umemuona mtoto wa Nabi (Hedi) tulirudi naye alikuja kutoka kwao akafikia Algeria akaangalia na mchezo na ujio wake ni pamoja na kusimamia hii hatua ya kusaini mkataba mpya wa kubaki zaidi Yanga.

“Niwatoe hofu Wanayanga kwamba Nabi Yuko hapa kwa kubaki zaidi kuendelea kukisuka kikosi chetu.”

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMAMOSI