Home Uncategorized WACHEZAJI KUPIMWA CORONA MARA MBILI KWA WIKI

WACHEZAJI KUPIMWA CORONA MARA MBILI KWA WIKI


TIMU zote 20 zinazoshiriki Ligi Kuu England kwa sasa wachezaji pamoja na viongozi watalazimika kupima Virusi ya Corona mara mbili ndani ya wiki moja ili kuendelea kukabiliana na maambukizi mapya ya Corona.

Hali hii imekuja kutokana na maambukizi ya Corona kuzidi kuwa na kasi ambapo hivi karibuni iliripotiwa visa jumla ya 36 kwa waliopimwa ikijumuisha wachezaji pamoja na viongozi ndani ya timu shiriki.

Imeripotiwa kuwa ndani ya mwezi Januari jumla ya vipimo 2,593 kati ya Januari 4 na 10 vilifanyika  na maambukizi yameonekana kuwa kwa asilimia 1.39 kwa waliopimwa.

Mpaka sasa kutokana na janga la Corona jumla ya mechi tano za Ligi Kuu England zimesimishwa kutokana na kuchukua  tahadhari dhidi ya Janga la Corona ikiwa ni pamoja na ile iliyotarajiwa kuchezwa Januari 13, kati ya Aston Villa dhidi ya Spurs.

Pia kikosi cha Aston Villa kwenye mchezo wa Kombe la FA dhidi ya Livelpool wakati ikipoteza kwa kufungwa mabao 4-1 kwenye Uwanja wa Villa Park ililazimika kuwatumia wachezaji wake chini ya miaka 23 na wale wa chini ya miaka 18 kucheza mchezo huo kutokana na baadhi ya wachezaji wao pamoja na wafanyakazi wengine kuwa na Corona.


SOMA NA HII  MASHINE MPYA SIMBA YAPANIA KUFANYA MAKUBWA