Home Uncategorized MKUDE KUIKOSA RUVU SHOOTING TAIFA

MKUDE KUIKOSA RUVU SHOOTING TAIFA


JONAS Mkude, kiungo mkabaji wa Simba atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa wiki mbili baada ya kupata majeruhi kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya KMC.

Mkude aliumia mguu baada ya kugongana na mchezaji wa KMC, Kelvin Kijiri, Uwanja wa Simba Mo Arena Juni 8.


Akiwa nje ya uwanja Mkude ataendelea na mazoezi mepesi pamoja na matibabu ambapo ataukosa mchezo wa Juni 14 dhidi ya Ruvu Shooting.


Kwenye mchezo huo Simba ilishinda mabao 3-1.

SOMA NA HII  SUALA LA KUCHEZEA WANAWAKE, DIAMOND APEWA ONYO